Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts
Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts

Thursday, 16 July 2015

ZANTEL YATOA MSAADA WA VYAKULA KWA JUMUIYA YA WAZEE ZANZIBAR



Na Haroub Hussein


 Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imetoa msaada wa vyakula kwa ajili ya mwezi wa Ramadhani kwa makundi maalumu ya wazee hapa visiwani Zanzibar.

Msaada huo unajumuisha sukari, unga wa ngano pamoja na mchele umetolewa katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo.

Kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar imeainisha wazee zaidi ya 120 wenye uhitaji wa vyakula kwenye mwezi huu wa Ramadhani walio chini ya jumuiya ya wazee hapa Zanzibar.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa wazee, Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel-Zanzibar, bwana Mohammed Mussa, amesema ni kawaida kwa kampuni ya Zantel kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii katika kipindi hiki cha Ramadhani.


'Tuna furaha sana leo kuweza kusaidia jamii hii ya wazee ambao mara nyingi wamekuwa wanasahaulika, kwani tunaamini wazee ni sehemu muhimu sana ya jamii ndio maana Zantel leo tumeamua kutoa msaada huu ambao unatutofautisha sana na makampuni mengine katika vipaumbele vyetu' alisema Mussa.

Mussa aliongeza kuwa kama kampuni ya simu inayoongoza Zanzibar, Zantel mara zote imekuwa mfano katika shughuli zake za kijamii na vipaumbele vyake kiujumla.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, mgeni rasmi ndugu Msham Abdallah, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar, alisema anaipongeza Zantel kwa kushirikiana na serikali kuyasaidia makundi ya wazee.


‘Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kulisaidia kundi hili la wazee, kwahiyo ni furaha kwetu leo kuona Zantel imekuwa ya kwanza kusaidia kundi hili leo’ alisema bwana Abdallah.

Akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya Zantel, naibu mwenyekiti wa jumuiya ya wazee Zanzibar, Bwana Mwadini Kutenga, alisema anawashukuru Zantel kwa msaada huo, akisema umekuja kwa wakati mufaka hasa ukizingatia kuwa wanakaribia kuadhimisha sikukuu ya Idi.

'Kwa misaada hii, Zantel inawafanya wazee nao wajiskie sehemu ya jamii, kwani mara nyingi wamekuwa wakisahaulika sana na kwa hakika hatutawasau kwa ukarimu wao huu' alisema bwana Kutenga.


Kampuni ya Zantel imekuwa msitari wa mbele katika kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani, na msaada huu ni maalumu kwa kundi la wazee ambalo mara nyingi linasahaulika katika jamii.

Jumuiya ya Wazee Zanzibar (JUWAZA) ilianzishwa mwaka 2013 ikiwa na lengo la kuwaunganisha na kuwasaidia wazee Zanzibar na sasa ina wanachama zaidi ya 1000.





Friday, 12 June 2015

BALOZI SEIF: DUMISHENI NIDHAMU KWENYE MICHEZO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amehimiza umuhimu wa wanamichezo kuendelea kudumisha nidhamu michezoni ili kulijengea sifa
Bora Taifa katika sekta hiyo kwa kuwa na wanamichezo walishiba maadili na heshima iliyotukuka.

Balozi Seif Ali iddi alitoa himizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na wachezaji pamoja na Viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambno } katika hafla ya kukabidhiwa Kikombe cha ubingwa baada ya Timu hiyo kupanda Daraja la kwanza Kanda mwaka huu.
Alisema nidhamu na heshima ndio kitu pekee kilichosababisha wachezaji wa enzi zilizopita hapa Zanzibar kuwika na hatimae kuiletea sifa Zanzibar katika ulimwengu wa kabumbu.

Balozi Seif alieleza kwamba Vijana wa sasa wana nafasi pana ya kuendelea kujifunza mbinu mbali mbali za michezo na hatimae kuwa mastaa ambazo hupatikana kupitia kwenye vipindi vya Televisheni pamoja na mitandao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wachezji pamoja na Viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe kutokana na kazi kubwa waliyoifanya na hatimae kuchukuwa ubingwa kwa kuingia daraja la Kwanza Kanda.

Balozi Seif alisema juhudi za wachezaji hao kwa upande mwengine zimeanza hatua mpya ya kujijengea uwezo wa kupata ajira kupitia mchezo wa soka ambao unaonekana kupendwa sana Duniani.

“ Wapo wachezaji maarufu wanaochezea timu zinazotajika Duniani katika ulimwengu wa kabumbu ambapo wengine wanatokea hata mataifa ya Afrika yanayolingana kiwango cha soka na Tanzania “ Alisema Balozi Seif.

Katika kuunga mkono wanamichezo hao wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe Balozi Seif ameahidi kuisaidia Timu hiyo Seti mbili za Jezi pamoja na Mipira Minne na akawataka wajiwekee malengo zaidi ya kufanikiwa katika fani yao hiyo kwa siku zijazo.

“ Wale Jamaa wakikuoneni mnavyolisakata soka sawa sawa kikweli watafikia hatua ya kukununueni tuu na kwa upande mwengine Zanzibar tutakuwa na haki ya kujigamba kwamba tumetoa wachezaji wanaouwezo wa kuchezea timu za Kimataifa “. Alisema Balozi Seif.

Akizungumzia suala ya ujenzi wa Jengo la kudumu la Timu hiyo ya Taifa ya Jang’ombne Balozi Seif aliwashauri Viongozi na wachezaji hao kuanza ujenzi wa msingi na yeye atakuwa tayari kusaidia matofali kwa hatua ya kunyanyua.


Alisema uwezo wa kujenga jengo lao uko mikononi mwao ambapo viongozi wao jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wanasaidia nguvu na maarifa ili kuona malengo waliyojipangia yanakwenda hatua baada ya hatua.

Mapema Rais wa Timu ya Soka ya Taifa ya Jang’ombe Salim Ridhiwani alisema Uongozi wa Klabu hiyo umeamuwa kuimarisha Timu hiyo ili kurejesha heshima na hadhi ya klabu hiyo iliyopotea katika miaka ya hivi karibuni.

Ridhiwani alisema Wanachama wa klabu hiyo wanajivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya klabu hiyo hasa kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuiwezesha timu yao kuyakabili mashindano makubwa ya Kombe la Mapinduzi na kutoa upinzani mkubwa kwa timu zenye uzoefu wa mashindano ya soka Kimataifa.

Naye Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed Said Dimwa alisema Uongozi wa Jimbo hilo umeifufua tena Timu hiyo ndani ya Kipindi cha miaka Miwili iliyopita baada ya kufifia kutokana na changamoto kadhaa zilizokuwa zikiikabili timu hiyo katika miaka ya nyuma.

Dimwa aliahidi kwamba yeye pamoja na viongozi wenzake watasimama imara katika kuhakikisha Timu hiyo inarejea katika hadhi yake iliyopewa na wapenzi wa timu hiyo ya kuitwa wakombozi wa Ng’ambo.

Timu ya Taifa ya Jang’ombe { Wakombozi wa Ng’ambo } ilipanda Daraja na kushiriki mashindano ya Daraja la Kwanza Kanda mwaka huu baada ya kuifunga Timu ya Soka ya Maungani Goli 1-0 katika mchezo wa Mwisho wa mashindano ya Ligi Daraka la Pili.







Thursday, 11 June 2015

WANAHABARI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO ILI KUDUMISHA AMANI


WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuacha kuandika habari ambazo zitakazosababisha kusababaisha vurugu na kuondosha amani iliyopo nchini Tanzania hasa  katika kipindi cha uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (ZAMEWO) Maryam Hamdani, wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari juu ya haki za binadamu na sharia za waandishi,huko katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba nchi kadhaa duniani zimekuwa zikitokea kwa fujo kutokana na wanahabari kuandika habari ambazo zinahamasisha kwa wananchi kufanya vitendo ambavyo husababisha kuvunjiika kwa amani.

Alisema kwamba si vyema kuonekana nchi kama Tanzania ambayo ni nchi yenye amani kuharibika kutokana na maneno makali yanayozungumzwa na wanasiasa  na wanahabari kuyafikisha kwa jamii.

“Nakuombeni wanahabari wenzangu tuzitumie kalamu zetu kwa kuandika habari ambazo zitasaidia kudumisha amani iliyopo nchini kwetu na sio kuandika habari ambazo zitasababisha kuvunjika kwa amani,”alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha aliseleza kuwa chuki za wanasiasa na maneno ya hasira yanayotoka katika midomo ya viongozi hao wa kisiasa yakiandiikwa katika na kutangazwa katika vyombo vya habari yanaweza kusababisha hali ya hatari katika nchi.

“Katika kipindi kama hichi cha uchaguzi hutokea mambo mbali mbali na kauli za kutisha na za hasira kutoka kwa wanasiasa,hivyo nakuombeni kuacha tabia ya kuandiika maneno hayo ili Tanzania isije ikawa kama Burundi au nchi nyengine,”alifahamisha.

Hivyo aliwataka wanahabari hao kusaidia kuwaelimisha wananchi kuleta na kuiendeleza amani iliyopo hapa nchini pamoja kuielimisha Serikali kulinda amani iliyopo.


Mafunzo hayo ya siku mbili kwa waandishi wa habari yameandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikiana na Chama cha Waa ndishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA).