Friday, 11 July 2014

MAKALA

Mwezi wa Ramadhaan imeteremshwa Qur-aan
Jichumie fadhila za kusoma na kuhifadhi Qur-aan

QUR-AAN ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)   yaliyoletwa kama ‘Wahyi’ (Ufunuo) kwa Mjumbe wa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Mtume wa mwisho Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyoandikwa katika Misahafu, yanayorithiwa na vizazi kwa vizazi, yaliyonukuliwa kwa mapokezi mengi, kusoma kwake ni ibaada, ni yenye miujiza hata kama ni sura ndogo kabisa, na ni uongofu kamili wa watu wote.

MAKALA

Maalim Idriss ameacha misingi bora ya maisha ya dini ya kiislamu

ZANZIBAR ni moja ya nchi maarufu ambayo iliyotoa walimu, masheikh na wanazuoni wengi ambao wameweza kuitangaza nchi pamoja na kuwasomesha vijana wengi wa ndani na nje ya Zanzibar.
Kama utataja majina ya masheikh hao ambao wamekuwa vinara wa kusomesha elimu hiyo ya dini, basi huwezi kumaliza bila ya kumtaja Al-marhum Maalim Idriss.
Kufahamika kwake huko hakutokani jambo lolote isipokuwa kazi yake ya ualimu ambapo alifanikiwa kutoa taaluma ya dini ya kiislamu kwa vijana wengi. Miongoni mwao hivi sasa ni masheikh wakubwa wa kutegemewa katika jamii yetu.
Kutokana na kuwa ni mwanazuoni maarufu visiwani humu, Makala hii imefanikiwa kutafuta historia yake alipoanzia katika maswala ya kidini, mpaka Mwenyezi Mungu alipomuhitaji kiumbe wake.
Katika kipindi kama hiki  cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, marehemu alikuwa akisomoa hitma na utangulizi kabla ya kuanza kwa darsa katika msikiti Gofu.

Tuesday, 8 July 2014

MAKALA - HALED- MSOMI,MJASIRIAMALI ALIEJITUMBUKIZA KATIKA FANI YA SANAA YA FILAM



Na Aboud Mahmoud                                  
“Sanaa si uhuni sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyengine tena kwa nchi zilizoendelea kama Marekani wasanii ni kama tunu ya taifa thamani wanayopewa utaona hata kama wakija katika nchi zetu wana ushawishi mkubwa sana na watu,kwa hiyo heshima huanzia nyumbani,”.